SEHEMU YA TATU Baada ya dakika tatu tangu wakate kona gari ikasimama, Tina akamwona mama yake walipotazamana wakajikuta wanatabasamu, tabasamu lililoutangaza upendo wao. Japo macho ya mama yalikuwa, mekundu na yamevimba hali hiyo haikumshtua sana Tina. Tabasamu lile halikudumu sana, likayeyuka bila wao kujua kama limetoweka tayari na kuwa mshangao. Mshangao wao ukamezwa na vumbi kali lililotokana na breki kali za gari mbele ya nyumba ya mama yake huyo wa kufikia. Dereva aliyekuwa anasubiri malipo yake na yeye aliungana na wanawake hawa kushangaa lakini alikuwa ni Tina aliyezidi kushangaa zaidi baada ya wanaume waliojengeka miili kutoka katika ile gari aliyokuwa imehisiwa na dereva kuwa imewafungia mkia kumvamia na kumzingira. "Askari....upo chini ya ulinzi!!!" alipewa maneno hayo mafupi kisha bila kuuliza swali wakamtia katika bangili zisizopendwa na jinsia zote bangili hizi za rangi ya shaba zilibatizwa jina la 'pingu'. Kwa mara ya kwanza katika mikono ya Tina. Bila maelezo wala majibu ya maswali yake ya 'nimefanya nini' aliongozwa hadi katika gari waliyokujanayo. Mama damu ikawa nzito kuliko maji akawakimbilia polisi wale na kuwavamia akiwa na maswali mengi, hakujibiwa hata moja zaidi ya kusukumwa na kubaki akigaa gaa chini akilia bila msaada wowote. Dereva wa teksi hakukumbuka kama alikuwa anadai pesa ama la aliwasha gari lake akatokomea huku akiilani siku hii iliyoanza vibaya sana kwake. Aliondoka huku akiacha msiba mkubwa. Majirani ambao waliamkia kuzungumza habari juu ya msiba wa Steve sasa waliweka hayo makubwa yasiyowahusu wakavalia njuga suala hili zito linalowahusu la mama Tina!!!! ****** Kila aliyeingia mahabusu siku hiyo alikuwa na habari juu ya msiba wa Steve Marashi, kila mtu alikuwa na lake lakini kati ya hayo habari za mwandishi kuhusika zilikuwa zikitajwa. Bado Sam alijikaza asiweze kujiwazia mabaya aliamini alikuwa hausiki hivyo kwake yeye hiyo ni habari anayotakiwa kuiandikia makala na jamii iweze kusoma, mara moja moja alimlaani huyo mwandishi aliyehusika na mauaji hayo "Acha papara Sam, tulia ukitoka ufanye uchambuzi wa kina" Alijionya Sam baada ya kugundua alikuwa akilalamika bila kuwa na uhakika na malalamiko yake. Ile hali ya yeye kurudishwa rumande hata kabla ya kuandika maelezo ilimuacha katika kizungumkuti, awali aliwaza kuwa huenda muhusika amepatikana naye ataachiwa huru muda wowote lakini hadi kigiza kinaingia mambo yalikuwa magumu sana, aliendelea kusota mahabusu. Akiwa amekata tamaa kabisa Sam alijitafutia kikona kizuri kabisa ambacho aliamini kuwa kitamfaa kwa usingizi wake hadi asubuhi ambapo aliamini kuwa lazima apate muafaka wa kwa nini anakaa rumande siku zote hizo bila kuufahamu mustakabali wake, akiwa hajaandika maelezo wala kufafanuliwa kwa kina kosa lake. Hakujua usingizi ulimpitia saa ngapi na hakujua hata huo muda aliamshwa ilikuwa saa ngapi. Alitolewa nje ya chumba cha mahabusu na kupelekwa sehemu nyingine kabisa ambayo haikuwa na mwanga wa kutosha. Huko aliwakuta watu wawili, mmoja akijitambulisha kama mfuasi wake wa siku nyingi katika habari huku mwingine akiwa ni mpelelezi wa kesi yake. Hapakuwa na mazungumzo marefu sana bali huyo mfuasi ambaye alikuwa mnene wa umbo alikuwa amekuja kumwekea dhamana Samwel, dhamana katika kosa ambalo halijui, dhamana hata kabla ya kuandika maelezo. Kidogo Sam aikatae dhamana ile lakini alijihisi kama anataka kufanya kosa la kuukataa uzima wa milele tena katika mtindo wa ofa. Pia maumivu ya mbu wakali wasiokuwa na huruma waliomshambulia akiwa mahabusu nao walikuwa sababu ya kujikuta anapokea dhamana isiyoeleweka eleweka. "Kaka Sam," alinong'ona yule mfuasi huku akimuinamia Sam sikioni, baada ya kugundua anasikilizwa akaendelea, "Nimejitoa mhanga hapa kukusaidia rafiki yangu ili na wewe unisaidie na ujisaidie mwenyewe, kuwa makini!!!" "Kivipi tena?'' alihoji Sam ambaye alikuwa peku huku nguo yake ikiwa imelegea kiunoni. Hakuwa na mkanda wala viatu. "Ukitoka hapa utajua. Tafadhali kuwa makini!!!" alihitimisha yule bwana ambaye Sam alijaribu kumtambua bila mafanikio. Wakati huo mpelelezi wa ile kesi alikuwa mbali kidogo hakuweza kuyasikia maongezi haya. Sam japo hakuridhika na lile jibu bado alihitaji sana kuwa huru hivyo alifanya kama ameelewa ili maongezi yasiwe marefu. Usiku huo baada ya Sam kurudishiwa saa na vitu vyake vingine anagundua kuwa ilikuwa yapata saa nane na nusu usiku. Alikuwa na akiba ya pesa, pia alikuwa na kadi ya benki. Aliachiwa huru akatoweka pale bila kujua ni wapi aelekee. Akiwa nje ya kituo kile cha polisi akakumbuka mara ya mwisho kabla ya kufika hapo alikuwa mapumzikoni na mpenzi wake Tina. Tina ambaye walikuwa na ahadi ya kuoana katika siku za karibuni. Sam akajenga tabasamu hafifu, akaona ni vyema ampigie simu Tina ili aweze kufahamu ni wapi alipo aweze kwenda. Alipopiga simu ikawa inatumika. Wivu ukapenya kama kisu kikali katika ngozi ya mwanadamu. Sam akauma meno, akaitazama saa yake Saa tisa usiku!!!! Anaongea na nani sasa hivi?? alijiuliza kwa sauti ya chini kisha kama vile aliyemkosea alikuwa mbele yake, Sam alipiga teke kopo tupu la maji lililokuwa limetelekezwa barabarani hapo. Kopo likapiga kelele za uchungu Sam akajikuta anashtuka mwenyewe alikuwa anataka kuingia katika hali ya kutaharuki akajiminya minya kichwa chake katika hali ya kuzuia taharuki hiyo. Alipojaribu tena na tena hali ikiwa ile ile, aliamua kumtumia ujumbe Tina. Ujumbe ule sio tu ulikuwa ukielezea mchomo wa wivu ulivyompiga bali pia ulikuwa unaandamana na hasira na kero kwa kutopokelewa simu yake. Alipomaliza kuandika ujumbe ule akamkumbuka mama yake Tina wa kufikia. Akawaza kama ni sahihi kumpigia simu ama la kwa muda huo. Wivu ukamjibu kuwa ni sahihi, akatafuta jina kwenye simu kwa jinsi alivyohifadhi hakuliona, akatafuta tena hakufanikiwa kitu. Akaamua kumtumia Tina ujumbe ule!!! Ilikuwa kitendo cha sekunde kadhaa mlio ukajibu, Sam akahisi ni taarifa ya kupokelewa ujumbe alioutuma kwa Tina (deliver report). Akabaki kusubiri majibu bila mafanikio, akataka kupiga tena simu, akakutana na ujumbe kutoka katika simu yake, namba iliyotuma ujumbe ule ilifanana kwa kila kitu na namba ya Tina, Sam akayalalamikia masikio yake kwa uziwi wa kijinga. Aliyalaumu kwa kutousikia ujumbe ule ukiingia, taratibu Sam akaufungua na kuanza kuusoma, kama ujumbe ule haukuwa nakala ya ujumbe alioutuma yeye basi ulifanana kila kitu na maneno aliyomwandikia Tina. "Tina ananirudishia meseji niliyomtumia????" alitahamaki Sam, alipoitazama tena simu aligundua kuwa alikuwa anatetemeka. Kusalitiwa ukawa wasiwasi wake wa kwanza, Tina alikuwa anamsaliti na ujumbe huo ameutuma bwana ambaye wako naye kitandani ama chumba kimoja muda huo. Sasa hakujiuliza mara mbili mbili, akaamua kumpigia mama Tina simu kwa kuziandika namba zake ambazo alikuwa amezikariri, jina 'Mama' likatokea katika kioo cha simu, Sam akajiuliza neno mkwe lililokuwa mbele ameliondoa nani, lakini hakujali sana mama na mama mkwe wote ni mama tu!!. Simu iliita lakini haikupokelewa. Sam akazimisha simu yake akachukua usafiri na kuelekea nyumbani kwake maeneo ya Yombo dovya wilaya ya Temeke. Kabla hawajafika mbali sana alimsishi dereva wa teksi asimamishe, akachukua bia mbili za kopo akaingia nazo garini akawa anagida taratibu huku akipiga miluzi isiyomaanisha wimbo wowote. Alimlipa mwenye teksi ujira wake, akazunguka nyuma ya nyumba ambapo huweka funguo wake wa ziada. Akaingia ndani akavua nguo zile chafu akaingia maliwatoni akajisafisha vyema kisha akajirusha kitandani, uchovu wa kulalia sakafu akiwa rumande, pombe alizokunywa kwa fujo zilishirikiana katika kumtia mwandishi huyu katika kifo cha muda. Usingizi wa pono!!!! * * * * * Saa nne asubuhi haja ndogo ndio ilimtoa kitandani Sam, alipomaliza haja zake alirejea tena chumbani alitamani kulala tena mara akaitamani na simu yake. Halafu ghafla usingizi ukakatika ghafla baada ya kuona santuli ya picha (VCD) ya moja kati ya filamu alizowahi kupewa na rafiki yake wa ukubwani waliotokea kushibana kiasi chake japo hawakuwa karibu karibu. Ilikuwa ni filamu ya 'MIUNGU SABA', iliyochezwa na kinara Steven Marashi. Ghafla kengele za dharula zikalia kichwani mwake, akakumbuka kuwa kuna habari za umauti kumkumba huyu swahiba wake, kitu ambacho hakukiamini mara moja lakini alikitilia maanani. Kama mkuki akachomoka akaiendea simu yake, akaiwasha ili aweze kupiga namba za Steve aupate ukweli kama alichokisikia akiwa rumande ni kweli ama tetesi. Wakati simu inawaka alikuwa akizitafuta namba za Steven katika kijitabu alipozinukuu maana Steve alikuwa mahiri sana wa kubadilisha namba za simu kutokana na usumbufu aliokuwa akiupata chanzo kikiwa umaarufu. Akiwa katika kutafuta simu ikaita, akaikimbilia kupokea akiamini kuwa ni Tina. Hakuwa yeye alikuwa mama yake na Tina. "Shkamoo mama!!" alisalimia Sam. "Marahaba nani wewe?" upande wa pili ulihoji. Mama naye ina maana amefuta namba yangu!!! alijiuliza Sam kabla ya kujibu. "Mimi Sam mama!!" "Samwel mwenzako amefanya nini tena mbona hivyo? Na yuko wapi sasa hivi?" "Mimi ndio nikuulize wewe mama..." "Uniulize mimi tena wakati hajazungumza na mimi polisi wamemkamata tangu jana asubuhi!!" "Polisi!!! wapi na saa ngapi?" Sam aliuliza akiwa ametaharuki tayari. "Kwani wewe hiyo simu yake amekupa saa ngapi Sam....ujue unanitania wewe mtoto" Mama Tina akaanza kuwa mkali. "Simu gani mama tena?" "Sam mwanangu naomba uweke kando utani...Tina yupo wapi kama upo naye niambie nisije kufa kwa presha mimi" "Mama sipo na Tina mimi..." "Na hiyo simu!!!" "Ni yangu....hii mama" Mama Tina akatukana tusi la kikabila chao kisha akakata simu. Sam akasahau yanayomuhusu Steven Marashi, sasa yakazuka ya mama. Simu...simu mbona ni ........Mungu wangu!!!!! akashtuka Sam baada ya kuutazama ule mkanda wa ile simu haukuwa wa kwake. Ilikuwa ni simu ya Tina kumbe muda wote alikuwa anajipigia simu, alikuwa anajitumia ujumbe na kukasirika pasipo sababu!!!. HILA!!!! akashtuka Sam. Tina mikononi mwa polisi!!! kidogo afikirie kurudi kule polisi aulizie lakini maneno ya tahadhari kutoka kwa mtu asiyemfahamu yakamtia wasiwasi. "Kuwa makini!!!! Kuwa makini!!!!" Sam akaamua kutuliza akili yake akautafuta umakini alioambiwa!!!! Akiwa katika kutafuta simu ikaita, akaikimbilia kupokea akiamini kuwa ni Tina. Hakuwa yeye alikuwa mama yake na Tina. "Shkamoo mama!!" alisalimia Sam. "Marahaba nani wewe?" upande wa pili ulihoji. Mama naye ina maana amefuta namba yangu!!! alijiuliza Sam kabla ya kujibu. "Mimi Sam mama!!" "Samwel mwenzako amefanya nini tena mbona hivyo? Na yuko wapi sasa hivi?" "Mimi ndio nikuulize wewe mama..." "Uniulize mimi tena wakati hajazungumza na mimi polisi wamemkamata tangu jana asubuhi!!" "Polisi!!! wapi na saa ngapi?" Sam aliuliza akiwa ametaharuki tayari. "Kwani wewe hiyo simu amekupa saa ngapi Sam....ujue unanitania wewe mtoto" Mama Tina akaanza kuwa mkali. "Simu gani mama tena?" "Sam mwanangu naomba uweke kando utani...Tina yupo wapi kama upo naye niambie nisije kufa kwa presha mimi" "Mama sipo na Tina mimi..." "Na hiyo simu!!!" "Ni yangu....hii mama" Mama Tina akatukana tusi la kikabila chao kisha akakata simu. Sam akasahau yanayomuhusu Steven Marashi, sasa yakazuka ya mama. Simu...simu mbona ni ........Mungu wangu!!!!! akashtuka Sam baada ya kuutazama ule mkanda wa ile simu haukuwa wa kwake. Ilikuwa ni simu ya Tina kumbe muda wote alikuwa anajipigia simu, alikuwa anajitumia ujumbe na kukasirika pasipo sababu!!!. HILA!!!! akashtuka Sam. Tina mikononi mwa polisi!!! kidogo afikirie kurudi kule polisi aulizie lakini maneno ya tahadhari kutoka kwa mtu asiyemfahamu yakamtia wasiwasi. "Kuwa makini!!!! Kuwa makini!!!!" Sam akaamua kutuliza akili yake akautafuta umakini alioambiwa!!!! ******
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni