Jumamosi, 12 Desemba 2015

HADITHI RIPOTI KAMILI SEHEMU SABA

SEHEMU YA SABA Kuna wanaume wengi hujitamba kuwa wao wanawajua wanawake nje ndani huenda na wewe ni mmoja kati yao. Kama ni kweli wajiaminisha kuwa unawajua viumbe hawa nje ndani nachukua fursa hii kukupa pole.  Wanawake ni mfano wa kitabu kikubwa kilichosheheni kurasa nyingi zilizonakshiwa kwa maandishi madogomadogo tena yaliyoandikwa kwa lugha ya kigeni usiyoielewa hata chembe. Jiulize utawasoma vipi na kuwaelewa wanawake??? NA HII NI SEHEMU YA SABA....... “Tina nimevumilia mengi hadi leo hii ninapozungumza na wewe haya, mengine yanatia hata aibu kuyasimulia. Najisikia aibu sana kwa sababu tu niliujua ukweli huku nikiwa bado nakupenda sana, unaikumbuka safari yangu ya ghafla kwenda Kilimanjaro.... nilikuwa sina jiopya sana lakini nilienda kuupooza moyo wangu katika baridi lile maridhawa kutoka katika kilele cha mlima Kilimanjaro. Niamini mimi kuwa sikuwa na jingine zaidi ya hilo. Kuna mambo mengine unaweza ukamsimulia mtu akakuona wewe mjinga kupindukia, kuna jambo hata mama yako mzazi ukimueleza anaweza kukuona mtoto wake unaelekea kurukwa na akili kwa sababu tu hauchukui maamuzi ambayo angekuwa yeye angeyachukua. Na nd’o maana sikutaka kwenda kujipooza nyumbani kwa mama yangu, sikutaka kwenda kwa marafiki, sikutaka hata kwenda kwa ndugu na jamaa zangu wa karibu najua kuna siku uchungu ungenizidia na ningesema kila kitu, nikaamua niende Kilimanjaro mkoa ambao hapo kabla sikuwahi kufika, hivyo sikuwa na mtu ninayemtambua kule. Hii ilinipa sababu za kuendelea kuwa mvumilivu.. kila yaliponizidia nilikuwa najifungia chumbani na kulia sana... hiyo nd’o ilikuwa tiba pekee.” Nilisita na kumtazama Tina aliyeonekana kutoelewa sababu hasa ya mimi kusafiri hadi Kilimanjaro. “Tina unakumbuka nikiwa Kilimanjaro nilikupigia simu na kukueleza kitu gani mke wangu?” nilimuuliza. Akatikisa kichwa kuashiria kukubalia. “Sawa, nilikueleza kuwa Steven kijana aliyekuwa anatufugia kuku pale nyumbani aondoke ukaniuliza kwanini nimesema hivyo nikakueleza kuwa nilikuwa ndotoni wakati naongea na wewe yakaisha.... si kweli kwamba nilikuwa ndotoni. Nilikuwa na akili zangu timamu sema siku hiyo uchungu ulipitiliza hali yake ya kawaida nilium,izwa na hisia, nikajitazama mimi nilikuwa nina mapungufu gani haswa, kwabnza kufikia wakati ule pesa ya kuhonga msichana yeyote nilikuwa nayo na ulikuwa unajua kabisa maisha yetu yamebadilika nd’o maana hata tukaanza kufuga kuku, tukahamia nyumba kubwa ya kutosha na tukaanza ujenzi wa nyumba yetu. Lakini sikuona haja ya kujaribu ladha ya mwanamke wan je ulikuwa unanitosheleza sana, kilichoniumiza ni hali ya wewe kutoridhika, najua haujui kama niliwahi kuketi na Steven tukazungumza.....” nikasita na kumtazama Tina akinipigia magoti huku akinisihi nisiendelee kumuadhibu kwa maneno yangu makali. Alilia sana macho yakawa mekundu na yakiwa yamevimba sana..... nilijisikia vibaya kumuona vile lakini nilijitahidi huruma isinitawale. “Keti Tina, bila kuzungumza ninaweza kufa muda wowote. Niache tu nizungumze..... Nilizungumza na Steven akanieleza kuwa siku moja uliwahi kumkaribisha mwanaume pale nyumbani na sio yule mwanaume wako wa kwanza...... kuna kitu kisichokuwa cha kawaida Steven alikigundua na wewe ukafahamu kuwa amegundua. Ukamsihi asinieleze jambo lolote lile na yeye akakuopa sharti kuwa ili akutunzie siri basi lazima na yeye umpe anachotaka, na hapo akakuomba penzi lako. Tina ukasalimu amri mbele ya kijana yule eti na yeye ukamruhusu... tena wakati huo kaSonia kalikuwa kadogo kweli, hukukaonea aibu Tina?? Ama isiwe aibu, haukukaonea huruma kwa kitendo hicho.... ok nilisema sitaki useme lolote hadi nitakapomaliza naomba basi unieleze huyo mwanaume aliyekuja ukamuingiza chumbani kwangu ni nani??” nilikoea pale na kumtazama usoni. Huku akiwa anatawaliwa na kilio cha kwikwi Tina alinieleza mkasa wa kwenda kwenye harusi ya rafiki yake, harusi aliyoenda kinyemela pasipo kuniaga. Akanieleza kuwa akiwa huko harusini wakati wa kutoka akaibiwa pochi yake, na mbaya zaidi hakuwa na mwenyeji zaidi ya shoga yake huyo ambaye alikuwa amelewa vibaya mno akiwa hajielewi kabisa, katika hangaika ya hapa na pale ndipo akakutana na mmoja kati ya washiriki katika harusi hiyo, akamuombea lifti kwa rafiki yake, kweli akapata lifti....  akamueleza huyo bwana sehemu aliyokuwa anaishi jamaaakamueleza hakuna shida ila kuna kifaa fulani lazima akipitie mahali na ndipo atampeleka nyumbani.... mwenye chake muheshimu Tina hakuwa na kipingamizi, wakaenda nyumbani kwa huyo bwana, baada ya kuchukua kifaa na kukifunga garini kama alivyoongopa eti gari likagoma kuwaka, na hapo ilikuwa tayari saa nane usiku.  Nikamkatisha Tina asiendelee kusimulia kisa kile kwa sababu tayari nilikuwa nimeanza kuupata mwanga. “Oooh! Ni siku hii ambayo ulirejea asubuhi ukaniambia kuna rafiki yako alizidiwa ukampeleka hospitali?” nilimuuliza huku nikilazimisha tabasamu lakini moyoni ikiwa ni hasira inanichemka. Tina akatikisa kichwa kukiri.... Ndugu msikilizaji na msomaji wa ripoti hii, licha ya kuwa mwanamke aliletwa kuipamba dunia na pia kuwa ubavu wetu wanaume. Mwanamke alibarikiwa kitu kingine cha kushangaza, mwanamke akiamua kabisa kukuongopea anakuongopea na unakubaliana naye kabisa, sijui ni ile sauti yao bembelezi waliyobarikiwa nayo, sijui ni yale macho yao ya kurembua waliyotunukiwa?? Lakini hakuna kiumbe mwenye ushawishi wa haraka kama mwanamke!!  Yaani siku ambayo Tina aliniongopea kuwa anatokea kwa rafiki yake, nilimuamini sana na nilimpa pole ya dhati kutoka katika sakafu ya moyo wangu kisha nikamkumbatia kwa nguvu, nakumbuka hata neno nililomueleza siku ile. Nilimwambia kamwe aischoke katika kutenda mema... akajibu AMINA!! Kumbe alikuwa amebeba siri nzito sana..... “Tina usijiulize nimeyatoa wapi mashaka hadi kufikia kuujua mkasa wa Steven kijana wetu wa kufuga kuku. Sikuwahi kukueleza ila ni kwamba siku kadhaa baada ya tukio lile na niliposhiriki na wewe tendo la ndoa, nilianza kupatwa na muwasho jambo ambalo si kawaida kabisa kwangu na si la kawaida kwa sababu nacheza mchezo salama nikiamini na wewe mwenzangu upo hivyo....... sasa Tina mpenzi wangu yaani kweli ikatokea bahati mbaya basi ukafanya zinaa na huyo mwanaume ama na hao wanaume yaani hata kuwakumbusha kutumia kinga mpenzi wangu huwakumbushi. Hivi ungeniambukiza Ukimwi mtoto wa watu mimi leo ungewaelezaje wazazio wangu labda... nambie ungewaelezaje wakuelewe!!! Nilienda kwa daktari baada ya miwasho ile akanieleza ni dalili ya gonjwa la zinaa, nikamueleza naambukizwaje labda akanieleza gonjwa la zinaa haliambukizwi kwa kugusana migoni, linaambukizwa kwa kuifanya zinaa yenyewe. Akanieleza huku akitabasamu. “Sasa bwana we naona pete kidoleni si una mke wewe?” nikamjibu ndio. “Achana na hizi mechi za ugenini mkuu, watakuharibia hawa. Tulia na mama watoto....” alimaliza daktari yule huku akinielekeza chumba cha sindano. Baada ya huduma ile ndipo akili yangu ilipoanza kuniwasha huku ikitaka majibu ya upesi sana, maana mimi nilikuwa  ninao uhakika kuwa sijacheza mechi za ugenini kama alivyosema daktari basi kama sio mimi basi Tina amecheza na mwisho ndo huu kuniambukiza..... nilighadhabika sana Tina na kama unayo kumbukumbu vizuri kuanzia wakati huo nilianza kutumia kinga nikiwa na wewe ukaniuliza sababu nikakuambia sitaki tupate mtoto wa pili wakati Sonia angali mdogo sana. Wala hilo halikuwa tatizo, tatizo lilikuwa moja tu nilikuwa nahofia unaweza kuniua, kuanzia hapo ndoa yetu tamu ikageuka vita vya kimyakimya...... **Ni Ripoti kamili iliyofanyiwa utafiti wa kina, jiulize nini mwisho wa ripoti hii......... je ungelikuwa wewe ungelifanya nini?? Usikose muendelezo wa mkasa huu wa mapenzi.....

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni