Jumamosi, 12 Desemba 2015

HADITHI RIPOTI KAMILI SEHEMU YA SITA

SEHEMU YA SITA WATU wengi huikosa furaha kwa sababau hawatambui kuwa ili uipate furaha iliyokamilika huna budi na wwewe kuwapa furaha wengine wanaoihitaji..... lakini wapo wanaojitahidi kadri wawezavyo kuwapatia furaha watu wengine tena watu wao wa karibu kabisa lakini badala ya kulipwa furaha wanalipwa huzuni..... maisha ndivyo yalivyo hayana usawa siku zote!! NA HII NI SEHEMU YA SITA....... Nilikuwa namuonea huruma sana Tina, nilijua ni kitu gani kinafukutika katika moyo wake, alikuwa anafanania na mtu anayeomba wakati urudi nyuma aweze kurekebisha popote alipokosea lakini kamwe wakati haurudi nyuma.  Nilijizuia nisimtazame Tina kwa jicho la huruma na badala yake nikajikaza na kuendelea kutoa ripoti ile iliyonigharimu muda na pesa nyingi katika kuifanyia utafiti na kisha kuiandaa. “Tina ulikuwa unajisikiaje ulipokuwa unaniigizia eti ile mimba ya Sonia ilikuwa imenichukia, kila kitu nikifanya kwako kinakuwa si sawa hadi ukaomba ruhusa kwenda kwa ndugu zako, eti ukiwa na macho makavu kabisa ukasema unaenda kwa bibi yako.... dada yako yule shetani aliyevikwa ngozi ya mwanadamu ili aweze kufanya vyema kazi yake na yeye akachochea kabisa huku akinibania pua. “Yaani sisi wanawake tuache tulivyo tu... wakati mwingine mimba inakataa ukoo mzima unashangaa inawapenda marafiki. Yaani Mungu anajua mwenye we alivyotuumba!!”..... Yaani Stela hakuona hata aibu kumtaja Mungu katika uongo huu unaofananishwa na kisu kikali, akamtaja tu hovyo kama kweli anamaanisha anachosema. Bwege mimi nikainama na kujichekesha nikakubali ukaondoka kwenda kwa bibi, bibi mwenyewe sasa nd’o huyo mwanaume wako....... eti mwanaume aliyekutoa usichana wako!!!  Tina yaani ukawa na amani kabisa upo na huyo mwanaume wako halafu ukawa kila muda unanipigia simu, nakumbuka kuna siku ukanigombeza kabisa eti inakuwaje nimechelewa kurudi nyumbani, tena ukalalamika kabisa kuwa unahisi siku hiyo nilikuwa namwanamke mwingine, basi mjinga mim,i nikakubembeleza wee nikikuomba uniamini... kumbe kilaunapokata simu unabaki kunicheka ukiwa na huyo mpenzi wako. Tina, hivi kweli mtu anayekupenda kabisa akubalikusikia unaongea na mwanaume mwingine usiku manenoya kimahaba???  Hakuwa akikupenda mwanaume yule.... na kukuthibitishia uchafu wake, yaani mdogo wake aliposafiri na kumwachia nyumba amlindie ndo akatuimia fursa hiyo kukualika wewe katika nyumba hiyo, we nawe ukajiona mama mwenye nyumba kweli. Unatia huruma sana Tina.... Zamani nilisikia kuwa marafiki wengi huchonganisha tu linapokuja suala la mapenzi lakini kumbe si kila rafiki ni mchonganishi, na marafiki wengine huogopa kabisa kumtoa ushauri linapokuja suala la mapenzi lakini shukrani za dhati kwa rafiki yangu aliyeamua kusema litakalokuwa na liwe lakini hawezi kuendelea kukaa kimya...... Akanieleza kuwa kuna mwanamke alikuwa anakuja nyumbani.... nilipuuzia awali lakini nilipofuatilia kwa ukaribu nikaugundua mchezo.. bwana yako alikuwa akitumia kivuli cha mwanamke kufika pale nyumbani, halafu yeye anakuwa garini. Huyo mwanamke anafika na kukuchukua mnaingia garini milango inafungwa halafu kifuatacho ni uchafu hata kusimulia. Na inaniumiza sana nafsi kwa sababu niliuona mchezo mzima kabisa, yaani ndani ya gari moja na mwanamke mwenzako anakushuhudia uchafu unaofanya na mwanamke huyo anajua kabisa wewe ni mke wa mtu!!! Haukuiogopa laana Tina wangu, yaani ujasiri mkubwa kiasi kile uliutoa wapi haswa. Natarajia majibu yako itakapomalizika ripoti hii nijue ni kitu gani kikubwa ulikuwa unapata hadi kukubali kudhalilishwa huku ukinidhalilisha na mimi...” nilisita na kumtazama Tina, alikuwa anatokwa jasho, nahisi alitegemea yote lakini hakuwahi kudhani kuwa nilikuwa nalala naye kitanda kimoja huku nikiyajua machafu haya aliyokuwa ameyahifadhi katika moyo wake akiamini kuwa ni siri. Ndugu msikilizaji mke anauma jamani...... namaanisha mkje ambaye kila anayekufahamu wewe basi anamfahamu na yeye kama ubavu wako, mwanamke unayelala naye kitanda kimoja ukimuamini kabisa kuwa ni mtu salama katika maisha yako unakuja kugundua kuwa vile anavyokukumbatia basi anamkumbatia mtu mwingine, vile anavyokuita majina ya kimapenzi basi kuna mtu mwingine pia anaitwa hivyohivyo. Ukiwa na moyo mwepesi unaweza kujikuta umefanya jambo baya sana ambalo utalijutia tena na tena. Naomba ninaposimulia ripoti hii wewe vaa viatu vyangu na ujiulize ingelikuwa wewe ungelifanya nini...... Nilipoona Tina anazidi kutokwa jasho niliwasha pangaboi nikaweka spidi ya kutosha tu ili aweze kupa ahueni, wakati huu Sonia alikuwa amesinzia tena. Baada ya kumpa pumziko hili nilirejea tena kwake...... kabla sijasema neno alinieleza kuwa ikiwa nina silaha yoyote ile basi nimjeruhi hadi afe ama kama nina sumu nimpe anye afe kwa sababu hana sababu hata moja ya kumuhalalisha kuishi. Nilimsogelea na kumvuta kwangu kisha nikamueleza kuwa sitamdhuru hata chembe, kama tulivyoingia ndivyo tutakavyotoka!!! Na hapo sikutaka upepo ubadilike na kuanza kuzungumzia hayo menghineyo nikarejea katika kijitabu changu kidogo nikafunua na kusoma alama nilizokuwa nikizitumia katia kuandika, na hapo nikapata jambo jingine la ajabu lakini  kutokana na kwamba nilifanya utafiti wa kina lilibakia kuwa la ajabu lakini la kweli. “Tina unaifahamu Doromee!!” nilimuuliza kwa utulivu kana kwamba hakuna kinachoendelea kati yetu. Akatikisa kichwa kupinga kuwa haijui.. Nikatabasamu kisha nikaendelea. “sasa Tina mke wangu wewe hata ungeweza kutumwa kuniua bado ungeniua tu.... sawa kwa sababu hauijui Doromee mimi ninaijua na nilifahamishwa na daktari, siku ile nilipochelewa kabisa kuamka halafu nikajikuta nikiwa nina homa kali sana. Kwenda kupima hospitali nikaambiwa siumwi na chochote... Tina awali nilihisi kuwa ripoti za daktari si sahihi lakini baadaye nikagundua kuwa ni sahihi, na aliyekutuma ni huyu mwanaume wako, akakutum,a uniwengee madawa hayo ili nipatwe na usingizi mzito sana unaodumu kwa masaa yasiyopungua kumi na mbili..... kweli kabisa mke wangu na wewe ukafanya kama alivyokutuma. Jiulize sasa ingekuwa ni sumu amekudanganya ni madawa ya usingizi.. hivi na wewe ungejiliza msibani na kugalagala katika kaburi langu huku ukilalamika eti mume wangu umeniacha na nani???? Sawa uliponiwekea yale madawa ulienda kwake au mlienda wapi?” nilimuuliza, sasa nilijisikia hasira ikinipanda sa. Huku akiwa anatetemeka vibaya mno alinijibu kuwa walienda nyumba ya kulala wageni. Nikamuuliza kuna jipya walienda kufanya ambalo hawakuwahi kulifanya siku za nyuma akasema hakuna jipya lolote walienda kuifurahisha miili yao. Nikataka kuongea nikajizuia maana koo lilikuwa limezibwa na donge la hasira, na nilivyojaribu kulimeza donge lile mara machozi yakaanza kunitoka. “Tina mke wangu, wewe ni wakala wa shetani!!!” nilimwambia huku nikishindwa kujizuia kulia kwa sauti.... Afadhali kwa kiasi fulani kilio kile kilinisaidia kwa kiasi fulani, koo likaachia na sasa nikakifungua kitabu kile na kuingia katiika ukurasa mwingine wa yote ambayo mke wangu aliyafanya huku mimi nikiwa sijui lolote... #Mkasa huu bado unaendelea, kuna mengi sana katika mkasa huu lakini ombi letu kwako ni kusikiliza huku unajifunza.... 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni