Jumanne, 15 Desemba 2015

RIPOTI KAMILI SEHEMU YA 20

SEHEMU YA ISHIRINI Na tena tusichoke katika kutenda mema na katu tusihesabu maovuya wenzetui ili kuukadiria wema wa kuwatendea..... malipo ya wema ni makubwa kuliko wema wenyewe!!!! Na hii ni sehemu ya ishirini!! “Tina.. ni nini hasa kilikusibu ulipokuwa Mwanza hadi ukaanza kunywa pombe na yote haya mapya ninayoyaona kwako....” nilimuuliza kiutulivu. Tina akaniuliza swali. “Mjuni una moyo mgumu sana natambua lakini sidhani kama upo tayari kulisikia na hili nqa kulipokea!! alijibu huku akinitazama. Nikamsihi sana kuwa nipo tayari kusikia jambo lolote lile... Tina akaniuliza mara mbilimbili kama nitaweza kuvumilia!! Swali hili la kujirudiarudia lilinitia mashaka kidogo japokuwa nilijiaminisha kwake kuwa nipo tayari kusikia na kupokea lakini kiukweli nilikuwa naogopa. Tina aliniomba niende nje kumchukulia maji anywe kisha tutazungumza vizuri. Nikaitazama saa yangu na kugundua kuwa ilikuwa yapata saa tano na nusu usiku tulikuwa tumezungumza kwa masaa mengi sana na bado yalikuwa hayajaisha mazungumzo yenyewe. Nilijipekua na nilipohakikisha kuwa ninayo pesa mfukoni nilimuaga Tina kwa kumbusu shavuni huku nikitoa tabasamu ambalo niliamini kuwa litamuongezea tumaini ambalo hakuwa nalo tena..... Njia nzima nilikuwa namfikiria Tina na kitu ambacho alikuwa anahitaji kunieleza, sikupata duka lililokuwa wazi nikawqauliza watu wachache niliokutana nao wakanieleza kuwa nizidi kwenda mbele kuna duka moja huwa linafungwa ikiwa tu mwenye duka ameamua lakini kwa masaa zaidi ya ishirini na mbili huwa lipo wazi.  Huo mwendo niliuona mrefu sana kwa sababu nilitamani tu kukaa pamoja na Tina ili anieleze ni jambo gani hilo zito ambalo alihitaji kunieleza na hapohapo akiwa amejawa na hofu tele kuwa sitaweza kulipokea. Hatimaye nililifikia lile duka nikanunua maji na kisha upesi nikaanza kutembea kurejea kule nilipomuacha Tina.  Nikiwa nimetembea mwendo mrefu kiasi nikakumbuka kuwa nimempa muuzaji noti ya shilingi elfu tano na katu hakunirudishia mabaki baada ya huduma ile. Nikasimama kidogo nikiwa katika kujiuliza maswali iwapo niiache tu ile chenchi ama niiruduie. Nikachekecha kichwa kidogo na hatimaye maamuzi yangu yakawa kurejea dukani kuitwaa iliyo halali yangu nikijisemea kuwa Tina yupo na ameamua kuwa na mimi usiku huo hivyo hakuna cha kuwahi!! Nikarejea dukani na kudai haki yangu nikapatiwa na kuondoka, lakini sikufika mbali tena nikaona banda la chipsi nikajisemea kuwa Tina wangu hakuwa amekula chochote zaidi ya zile pombe alizokuwa amekunywa hivyo lingekuwa jambo la hekima kumpelekea chakula pia. Naam! Nikaagizia chipsi mayai na mishkaki mitano kwa ajili yangu na Tina!! Huduma ilichukua muda kidogo kwa sababu moto ulikuwa umeanza kufifia lakini baada ya nusu saa hivi nilipata kuhudumiwa. Naam! Nikaondoka huku nikiwa na imani tele nafsini kwangu. Hatua moja ikifuatiwa na hatua nyingine nikakifikia kile chumba nilichomuacha Tina. Kilikuiwa tulivu kabisa kama nilivyokiacha tu, nami nikaingia kwa kunyata ili ule ukimya ubaki vilevile na kama Tina amesinzia basi nikamshtukize anikute nipo ndani ya chumba. Nikapiga hatua na kuingia ndani... kweli Tina alikuwa amwelala lakini hakuwa ametulia alikuwa akijirusha huku na kule mapovu yakimtoka mdomoni na macho yake yakigeuka huku na kule. Palepale nikauachia mfuko ule wa chipsi na kopo la maji, miguu na mikono ikiwa imekosa ushirikiano nilianza kutetemeka. Nikamfikia Tina na kuanza kumtikisa lakini mara nikaacha baada ya kugundua kuwa nilikuwa namwongezea mtikiso wakati alikuwa anatikisuika tayari. Hapo sasa nikajikuta natokwa na yowe kubwa sana la kuomba msaada. Yowe lile la kujirudia mara kwa mara linkawaamsha wateja na wahudumu wa nyumba ile ya kulala wageni. Hapo hekaheka zikaanza nikiwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa kila kitu kinakuwa sawa, Tina alikuwa amekunywa sumu!! Nilikuwa nahaha huku nikishangaa ni kwa nini Tina amekuwa na nafsi iliyojawa na ubinafsi kiasi hiki! Yaani licha ya kumsihi kuwa sina tatizo wala kinyongo naye bado ameenda kunywa sumu!! Nikakumbuka kuwa aliniambia kuwa jambo analotaka kunieleza ni zito sana na haoni kama naweza kuhimili kulipokea na kulihifadhi katika moyo wangu. Dah! Kumbe jambo lenyewe ndo hili, kujiua!! Hakika sikuwa tayari kulishuhudia na kulihifadhi moyoni jambo lile. Tina aondoke wakati Sonia naye ameondoka tayari...  Hapana haikuwa sawa hata kidogo kwangu.  Nilikuwa nalia kama mtoto wanaume wachache niliokuwanao katika hekaheka hizi walinitia moyo na kunieleza kuwa machozi hayasaidii kitu chochote badala yake nijikaze tu. Ndugu msikilizaji, waweza kuwa mmoja kati ya watu ambao huwatia moyo watu wengine lakini hakuna kitu kigumu kama kutiwa moyo katika mazingira kama haya, wale wanaokutia moyo unawaona kama wasioelewa hata kidogo jambo wanalokueleza. Na ndivyo ilivyokuwa hata kwangu. Ilikuwa ngumu kuwasikiliza watu hawa........ Tulipofanikiwa kumtoa nje kitu cha kwanza tulimlazimisha Tina kunywa maziwa akiwa hana fahamu sawia hivyohivyo kweli jitihada kiasi fulani zikazaa matunda akaanza kutapika na wakati huo teksi ikafika tukampakia hadi hospitali. Ni huko Tina alipoupata uhai tena na uhai huu ulikuja nikiwa pembeni yake.   ***** Punde baada ya kurejewa na fahamu Tina mtulivu kabisa alipepesa macho huku na kule....... kisha akakohoa kidogo na kunieleza. “Kwanini hamkuniacha nife... ni kitu gani unataka kwangu Mjuni. Niache Mjuni. Niache nife tu....” alizungumza kwa utulivu huku akipepesa macho huku na kule. Sikujali maneno aliyokuwa anasema Tina badala yake nilifurahia tena ule uhai wake na sauti kutoka katika kinywa chake. Hakika moyo wangu haukuwa tayari kushuhudia Tina akimfuata Sonia. Baada ya kimya cha muda kupita Tina alianza kuzungumza kana kwamba eneo lile yupo peke yake na hakuna anayemsikiliza. Ilikuwa sauti ya chinichini lakini niliweza kumsikia na kumuelewa kwa sababu chumba kilikuwa kimya sana. Alielezea juu ya safari yake ya Mwanza kisha akatajka majina kama ya wanaume sita tofauti na hapo akatikisa kichwa na kutabasamu peke yake. Akanieleza kuwa kamwe hakuwahi kujua eti ipo siku atapitia njia ya uchangudoa kwa hiari yake mwenyewe lakini akiwa jijini Mwanza huku akiwa na jeraha la kubakwa na kudhalilishwa alijikuta akiiona thamani yake haiishi tena katika ulimwengu huu na hapo lolote akawa anafanya. Akajiingiza katika ulevi uliokithiri, uvutaji wa sigara na hatimaye uchangudoa. Na hapo akauelezea kuwa huu ulikuwa mwanzo wa mwisho wa safari ya maisha yake... Akanigeukia akiamini kuwa sijaelewa lile neno lake  “Mjuni mimi ni wa kufa tu... nimeathirika Mjuni na sio jana wala leo.... nina miezi mingi tu na muda wowote ule nitakufa.” Tina alinieleza huku akitabasamu kwa kujilazimisha na macho yake yakilengwa lengwa na machozi. Nilidata ghafla na mwili wangu ukapooza sabna, nilihisi kiubaridi kikali sana kikipenya katika mwili wangu.  Tina akaendelea kuniomba sana msamaha na kisha akaniambia kuwa kama yawezekana nimpe tu sumu anywe kisha nimpe msaada wa kumzika.... Maneno haya ya Tina sikutaka kuyasikia hata kidogo hasahasa alipokuwa anazungumzia jambo la kujitoa uhai. Ni kweli alikuwa ameathirika labda lakini bado hiyo haikuwa sababu kuu ya kujitoa uhai...... Bila shaka alikuwa hajapata mshauri mzuri. Nilipiga goti chini kisha kimoyomoyo nikamuomba Mungu wangu kuwa iwapo nimekutana na Tina ili niwe nafasi ya pili katika maisha yake basi na anijaze nguvu lakini kama Tina ni shetani na nimekutana naye bahati mbaya nikamuomba Mungu aniepushie mbali huku nikikumbuka pia kumueleza Mungu ninayemuamini kuwa mitihani ya mateso niliyopitia inatosha aniepushe kama huu nao ni mtihani. Mungu ninayemuamini mimi anaishi, hilo ndilo ninaloliamini hadi wakati huu ninapokusimulia mkasa huu wa mapenzi. Niliamini pia katika ombi langu hili atanipa jibu stahiki kabisa ambalo litanifanya nisirejee nilipotoka. Naam! Asubuhi nikajisikia amani kabisa kuondoka pamoja na Tina na hapa tulienda moja kwa moja nyumbani kwangu...... Sikujua ni kipi nitafanya kwake angali amevikwaa virusi tayari lakini niliamini kuwa kadri ninavyopiga hatua moja mbele na ndivyo majibu yatakavyojileta yenyewe. Hatimaye hadi tukafika nyumbani kwangu...... Tina akawa mgeni wangu mgeni niliyeishi naye kwa tahadhari kubwa sana ili asije akajaribu kujiua ama kujifanyia lolote baya. Kwa juma moja niliishi naye huku nikijitahidi kumfikisha vituo vya ushauri nasaha, alipoimarika nikampangishia chumba chake mwenyewe eneo lisilokuwa mbali sana na nilipokuwa naishi. Nikampatia mtaji kidogo ili afanye biashara yake ya kumuingizia kipato, sikuwa na mashaka na uwezowake katika kupambana...... Naam! Maisha yakaanza upya yakiwa na tumaini tele upande wa Tina na tabasamu la kutosha kwangu mimi... Katika tumaini na tabasamu hili akaingiolia kati bwana mmoja aliyeitwa Abduli......... Huyu akauleta mwisho wa ajabu wa mkasa huu........ *Abduli alifanya nini... na mwisho upi anaouleta???? Usikose sehemu inayofuata ya mkasa huu wa RIPOTI KAMILI

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni