Rayvanny ft Diamond platinum -Mwanza
Salum Mazwazwa
Jumamosi, 10 Novemba 2018
Jumamosi, 1 Septemba 2018
Jumapili, 3 Januari 2016
HILA NO.13
HILA NO.12
Jumatano, 30 Desemba 2015
HILA NO.11
SEHEMU YA KUMI NA MOJA JOPO la madaktari wenye asili ya kihindi liliingia katika chumba cha ambacho Yakubu Gama alikuwa amelazwa. Walikuwa wameng’ara katika sare zao rangi ya bluu. Waliweza kuongea maneno machache tu ya kiingereza, asili yao ilikuwa uhindini. Baada ya kuingia katika kile chumba milango ilifungwa huku wakitoa agizo kuwa haruhusiwi mtu yeyote kuingia katika chumba kile. Askari wakabaki kufanya ulinzi! Baada ya milango kufungwa, daktari mmoja alitwaa simu yake na kupiga namba kadhaa, sekunde chache mbele simu ikapokelewa. “Tupo ndani ya chumba tayari!” alizungumza kwa kiingereza kibovu. “Kumbuka kufanya upesi na kwa usahihi kama nilivyowaeleza….” “Hakuna mashaka!” Akakata simu na kuwafanyia wale wenzake kama ishara! Wakakizunguka kitanda kama wakizungukavyo kitanda cha mgonjwa mahututi. Mgonjwa alikuwa ana majeraha makubwa ya kuunguzwa na moto na pia alikuwa amevunjika mkono na mguu. Naam! Gama aliyejeruhiwa katika mlipuko wa bomu. Wakamtundika mipira mingine katika mishipa yake na kisha kuruhusu dawa zimwingie kwa kasi. Wakati huohuo daktari mwingine akiuamsha moyo wa mgonjwa kwa kutumia mashine. Hatimaye akakohoa, wakaendelea na jitihada zao hadi fahamu zikamrejea. Wale madaktari wakafanya kama walivyoagizwa wakaanza kumuhoji mgonjwa kitandani. Maswali yao yote yalikuwa juu ya tukio lililopita na kumfanya awe pale kitandani hoi. Walimuuliza alichokuwa anakumbuka lakini hapakuwa na majibu, yule bwana hakuonekana kukumbuka jambo lolote lile. Walimuuliza jina lake akajitambulisha kuwa yeye ni Hasani Hasani. Madaktari waliyarekodi majibu yote hayo, kama walivyoagizwa kuwa kwa majibu yoyote atakayoyatoa yule bwana ambaye walimtambua kwa jina la Gama Yakubu. Baada ya kurekodi kilichokuwa kinafuata ni kuuondoa uhai wa mtu yule aliyesadikika kuwa na lolote ajualo kuhusiana na mkakati mahususi wa siri!! Naam! Wakamwondoa uhai wake kwa kumchoma sindano yenye sumu kali. Kisha wakatoka ndani ya kile chumba huku wakitikisa vichwa vyao. Wakasikitika na kutoa majibu kuwa haikuwezekana kuokoa uhai wa Gama kwani damu ilivilia katika ubongo wake. Pia wakasisitiza zaidi kuwa mwili wa marehemu umeharibika vibaya hivyo ni vyema uzikwe mapema. Taarifa za Yakubu Gama kupoteza uhai zikamfikia IGP na mrakibu msaidizi Robert. Kila mmoja akaipokea katika namna aijuayo mwenyewe. IGP akampigia simu mzee Matata na kumshukuru kwa jitihada kubwa alizoonyesha, akamsifu kwa uzalendo wake katika nchi isiyokuwa yake. Lakini hakusahau kumkandia bwana Robert kuwa kwa kuchelewa kwake kuwaruhusu madaktari basi amechangia kifo cha Yakubu Gama. Mwisho akamweleza Mzee Matata kuwa raisi atasimamia safari nzima ya madaktari wale kurejea nchini India. Mzee Matata akashukuru na kisha simu ikakatwa. Gama akahesabika kuwa kijana wa pili muhimu kabisa katika usalama wa taifa kupoteza uhai katika kipindi cha mwezi mmoja.. Mzee Robert alipewa taarifa ile ya kifo na mkewe kama ushuhuda juu ya alichomweleza usiku juu ya madaktari hao feki. Bwana Robert alimkumbatia mkewe na kumshukuru kwa ushauri wake lakini akabaki kusikitika kuwa yeye hakuwa juu ya IGP hivyo asingeweza kuwazuia madaktari wale kuingia katika kile chumba alichokuwa amelazwa Gama. Mke akatoa pole na kumtia moyo mume wake. Mzee Robert akashukuru! Na baada ya hapo akamuaga mkewe na kuelekea hospitali ya Lugalo. Huko akaenda kukutana na Daktari Macho. Bwana ambaye walisoma naye shule moja ya msingi hadi chuo kikuu, na hapo wakatengana mmoja akisomea udaktari na mwingine akisomea uhasibu! Taaluma zikawatenganisha lakini baadaye zikawakutanisha tena, Dokta Macho akiwa anafanya kazi katika hospitali ya jeshi na Robert akiwa na cheo cha Mrakibu mkuu wa polisi. Usiku ule thamani ya urafiki wao iliendelea kuonekana huku wakiwa wanaaminiana kwa silimia kubwa. Dokta Macho aliyasikiliza mashaka ya Robert na kuamua kutii alichosisitizwa, akamuhamisha chumba Yakubu Gama kisha katika kile kitanda akawekwa bwana aliyeshukiwa kuwa ni mwizi, wananchi wakachukua sheria mikononi na kumchoma moto. Lakini kabla mambo hayajawa mabaya sana akaponea chupuchupu na kuwahishwa hospitali. Majeraha katika mwili wake na yale ya Yakubu Gama baada ya mlipuko yalifanana sana maana yote yalikuwa majeraha ya moto. Wale madaktari kutoka India wakakutana na mchezo ndani ya mchezo waliopanga kuucheza. Wakachezewa shere na mwisho wa siku wakaumalizia uhai wa yule kibaka. Wakajisifu kuwa wamemuua Yakubu Gama. *** Kwa kitendo kile cha kuwarubuni madaktari, bwana Robert alitambua vyema kuwa amejiingiza katika vita na IGP pamoja na mkuu wan chi maana hawa walikuwa hawaambiliki kwa lolote juu ya mtu wa kuitwa mzee Matata. Hofu kubwa aliyokuwanayo Robert ni juu ya usalama wake na daktari aliyeshiriki katika tukio lile. Na hapo akatambua kuwa hatakiwi kulala kitandani na kupeleka mambo taratibu taratibu. Badala yake alitakiwa kufanya mambo kwa kasi ya ajabu ili hata siku wakimlaza usingizi wa milele basi neno lake liendelee kuishi huku likiwaumbua wote waliokuwa wakijificha huku kiuhalisia walikuwa wauaji. Kwa kufikiria ni namna gani anaweza kuchakarika kwa kasi bila uoga. Robert akaamua kuyahamishia mambo yaliyokuwa katika kichwa chake akayaweka katika maandishi. Neno kwa neno kuanzia mashaka yake juu ya mzee Matata, pia lawama zake juu ya IGP na kisha akagusa mamlaka kuu ndani ya nchi akapagusa Ikulu. Akapataja kuwa panahusika kumficha mzee Matata. Baada ya kuandika kurasa nyingi sana akautuma ujumbe ule mahali ambapo aliamini kuwa ni sahihi kabisa na wala hatakuwa amepotea kufanya vile. Hakujitambulisha yeye ni nani wala cheo chake katika uongozi wa jeshi la polisi. Harakati zikazidi kupamba moto!! ***** MOROGORO MJINI AKILI za kuzaliwa za Atuganile ama maarufu kama mama lao zilimfaa mara nyingi sana. Hata katika maisha yake ambapo alikuwa ameishia darasa la saba hakubabaika na kuyaogopa maisha. Alipambana kwa mafanikio jijini Mbeya na kisha kuingia jijini Dar es salaam huku akiwa hana mwenyeji hata mmoja. Lakini licha ya hayo bado aliweza kupambana bila kuwa ombaomba. Kilichokuwa kinambeba katika maisha yake ni siri zake kwa jambo ambalo anatarajia kulifanya. Kila wakati alikuwa akihofia kuwaambia watu mipango yake kwa kuhofia kukatishwa tama. Hivyo aliiongoza serikali ya maisha yake kwa kutumia kichwa chake mwenyewe. Tabia hiyo iliendelea hata siku ile ambapo alipandishwa gari na Sam kwa ajili ya kwenda Mbeya. Naam! Alihitaji Sam atambue kuwa yupo Mbeya, ili ikitokea siku moja Sam amekamatwa na kubananishwa ipasavyo ajikute akiisaidia ;polisi upelelezi wa kumtafuta mama lao Mbeya. Msako ambao ungewachukua miaka zaidi ya kumi bila mafanikio yoyote. Wangedumu wakimsaka mama lao jijini Mbeya wakati mipango yake ilikuwa tofauti kabisa. Mama lao kwa utashi wake mkubwa gari lilipofika Morogoro akashuka, bila kutoa taarifa. Gari likaondoka huku siti yake ikibaki wazi, kondakta akajisikia vibaya sana kuwa amemuacha abiria wa kwenda Mbeya stendi ya Msamvu Morogoro. Wakati kondakta akifadhaika na kumuuliza jirani yake juu ya yule abiria wa Mbeya aliyeachwa njiani. Mama lao alikuwa ameshikilia gazeti ambalo lilikuwa likimtangaza kuwa anasakwa kwa mauaji. Alitabasamu kisha akacheka kwa nguvu! Hakuwa na wasiwasi hata kidogo. Hakika alikuwa na jina kubwa lakini bahati nzuri iliyoje hakuwa na kumbukumbu ya kuwahi kupiga picha jijini Dar es salaam. Mazingira aliyofanyia kazi hayakuwa mepesi kupiga picha, alikuwa ni mtu wa kutingwa masaa yote. Nani angekuja kumpiga picha!! Ungekuwa mgahawa wa watu wa kifahari walau wangepata huo muda wa kuchukua kumbukumbu. Lakini waliohudhuria mgahawa ule wengi wao walikuwa mafukara tu ambao msongo wa mawazo ni kipande kimoja katika maisha yao ya kila siku. “Wali nyama, niwekee wa kushiba!” hizi nd’o zilikuwa lugha zao. Baada ya hapo ni malipo na kukutana tena ni kesho yake. Magazeti yakabaki kuandika jina la mama lao tu! Bila picha wala jina halisi hawakulijua. Tanzania nzima kuna akina mama lao wangapi?? Bahati iliyoje kwa mama lao Atuganile kuonyesha makucha yake pasipo kujulikana. ***** KATIKA Mji ambao aliishi mama lao kwa wakati ule, ulikuwa ni mji wa maficho pia kwa kijana Yakubu Gama ambaye alikuwa amehifadhiwa kwa ajili ya matibabu. Fahamu zilikuwa zimerejea tayari na damu yake ilikuwa inachemka haswa kwa ajili ya mapambano. Alikuwa na kiu ya kujua kunani hadi mambo haya yote yanatokea. Na kubwa zaidi alitamani kumjua muuaji wa Steven Marashi ambaye alikuwa pacha wake katika kazi kabla hajahamishiwa kazi maalumu ya upelelezi, kazi ambayo ilimfanya ajikute katika sanaa ya maigizo na hatimaye kuanza kucheza katika filamu. Hakuna hata muigizaji mmoja aliyetambua kuwa Steven Marashi alikuwa kijana wa usalama wa taifa. Kwa tukio lile la kulipukiwa na bomu ambalo lilikuwa katika mwili wa kijana aliyeagizwa na BVB kulizidi kumtamanisha kutambua kuwa ni kitu gani ambacho kinafichwa. Hisia zake kubwa zikajijenga juu ya upelelezi ambao Steven Marashi alikuwa akiufanya kimyakimya dhidi ya kigogo wa serikali. Upelelezi alioubatiza jina oparesheni tokomeza. Alichotaka kukitokomeza alifahamu yeye mwenyewe.. jambo la muhimu alimsihi Gama kuwa mtulivu ayangoje majibu. Hivyo kama Steve ameuwawa bila shaka ule upepelezi wake ambao alikuwa hajaukabidhi ofisi kuu ulikuwa katika mikono ya mtu mwingine ambaye amezing’amua siri nzito za usalama wa taifa. Kitendo cha kutaka kuuwawa akiwa hospitali kilimsababisha apigie mstari mashaka yake na kuamini kuwa anatakiwa apambane upesi ili kuupata ukweli. Na aliamini hilo linawezekana sana kwa sababu tayari alitambulika kuwa amekufa. Na vile mwili wake haukuagwa kwa sababu kuwa ulikuwa umeharibika sana. Akabaki kujulikana yu hai kwa watu wasiozidi wanne! Hakuna hata mmoja kutoka katika familia yake aliyetambua kama yu hai mjini Morogoro. Gama alijaribu kutembea kwa kujivutavuta hadi akakifikia kioo. Akajitazama! Lahaula! Hakuwa yeye, sura yake iliunda mfano wa mapunye na ngozi yake ilikuwa imechubuliwa vibaya sana na lile bomu. Akajaribu tena na tena kujitazama hakuwa yeye! Hasira zikamjaa kifuani akaubamiza ukuta kwa ngumi nzito! Na hapo mwenyeji wake ambaye ni daktari akaingia na kumsihi ajipumzishe kwani hakutakiwa kujihangaisha kwa lolote hadi pale atakapopona! Gama alirejea kitandani akajilaza lakini ni kwa kupumzisha mwili tu na sio akili. Akili ilikuwa inapanga mikakati kabambe! Akamfikiria sana hayati Steven Marashi, akakifikiria kifo chake kilivyokuwa cha upesi, na tetesi zake ambazo hazikuwa zinaeleweka. Mara ameuliwa kishirikia na mpenzi wake, mara amejiua. Gama akaufikiria ukakamavu wa Steve, akafikiria ni jinsi gani alikuwa na uwezo wa kupambana na maadui zake, akaitambua misimamo yake. Hapa zile tetesi za kujiua akazifutilia mbali. Akamkumbuka tena namna alivyokuwa bingwa wa mapambano ya ana kwa ana. Pia alivyoweza kupambana na mtu mwenye silaha…. Hakika Steven alikuwa mwiba! Kuhusu mtu yeyote kuweza kumuua kirahisi vile labda kwa kumnyonga ama kumpa sumu. Hili nalo akalifutilia mbali! Angeweza kufa mtu mwingine kizembe namna ile lakini sio Steve!! Gama alipingana kabisa na hisia za Steve kuuwawa kizembe. Mara ghafla akayafikiria MAPENZI. Na hapo akaketi kitako. Akajenga picha ya mfanyakazi mwenzake huyo ambaye tayari ni marehemu. Akamkumbuka jinsi alivyokuwa anakosa raha pale anapokerwa ama anapomkosea mpenzi wake. Alikuwa anashindwa kufanya kazi kabisa na wakati mwingine hata kufanya chini ya kiwango! Yawezekana mapenzi yamemuua Steven!! Gama alijisemea huku akitikisa kichwa chake kuuunga mkono hoja ile. “Lakini mapenzi kivipi?” akajiuliza…. Akawafikiria baadhi ya wasichana ambao walikuwa wakijihusisha kimapenzi na Steve. Mariam, Subira, Recho….. Akayamaliza majina yote yale aliyokuwa akiyafahamu, akampa kipaumbele Mariam. Huyu ndiye alikuwa akitumia naye muda mwingi mara kwa mara kwa sababu Subira na Recho hawa walikuwa wake za watu hivyo ndoa zao ziliwakosesha muda wa kuwa na Steve mara kwa mara. Lakini Mariam hakuwa ameolewa na mpenzi pekee aliyekuwanaye kiuwazi alikuwa ni Steve, penzi lilianza kwa kasi kubwa lakini baadaye penzi likashuka thamani, ikawa linapita hadi juma moja bila Steve kutoka na kwenda mahali na Mariam, lawama zikaanza na mwisho zikapoa. Mariam akawa hawezi tena kumwendesha Steve! Sasa nani alikuwa akimwendesha?? Akajiuliza! Huyu nd’o anayetakikana nijue nini kimemuua Steven Marashi! Hapa kama si mapenzi basi kuna HILA zimefanyika, aidha Mariam alimuua kulipiza kisasi ama.. ama….. Gama akakosa lolote la kutabiri! Akajipa siku tatu za ziada mbele ili aweze kuanza rasmi kazi nzito kupita zote alizowahi kufanya. Kujua ni kipi kimemuua rafiki yake na kuna njama gani zinaendelea asizozijua!! Kubwa zaidi kuhusu ripoti ya hujuma ambayo anaamini Steve alikuwa ama ameikamilisha ama alikuwa amekaribia kuikamilisha. Gama akatabasamu kisha akajilaza tena. Wakati huu ni mwili na akili. Akasinzia huku fikra ya mwisho kabisa akiwa amemfikiria mtu wa kufanya naye hiyo kazi. ***** MIAKA MINNE ILIYOPITA ILIKUWA imebaki miaka minne kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika tena. Chama tawala kilitarajiwa kusimamisha mgombea mpya baada ya yule wa awali kuwa anaelekea kumaliza miaka yake kumi kama katiba isemavyo hawezi tena kugombea. Anatakiwa kuwaachia wenzake. Tofauti na miaka mingine ambapo mgombea anaandaliwa mapema kabisa. Lakini hii ya wakati huu ilikuwa kinyume kabisa. Wagombea wenye sifa walionekana kuwa wawili na wote walikuwa wenye nguvu sana hivyo likawa ni jukumu la chama tawala kufanya uchaguzi sahihi ili nchi iendelee kuwa chini ya utawala wao. John Masele, waziri wa mambo ya ndani na nje ya Tanzania alikuwa ameitangaza nia yake mapema kabisa kuwa anataka kuingia ikulu. Wafuasi wake wakaanza kumuita raisi mtarajiwa, jina likazoeleka huku akionekana kukosa kabisa dosari yoyote ya kupata nafasi hiyo. John Masele alikuwa akikubalika hata kwa wapinzani, alikuwa na sera za peke yake ambazo zililenga katika kumkomboa mtanzania kiuchumi, kiutamaduni na kifikra. Raisi aliyekuwa madarakani hakufanana misimamo na Masele, hivyo alitambua wazi kuwa hataishi kwa raha tena wakati akiitwa raisi mstaafu. Alihofia bwana Masele anaweza kutumia utawala wake kumsababisha yeye aonekane hakuna lolote alilofanya wakati akiwa ikulu. Jambo ambalo kwake lilikuwa fedheha kuu. Raisi akamshawishi, Mathias Obhare, waziri wa nishati na madini atangaze nia ya kugombea pia. Huku akimsisitiza kuwa asimuhofie Masele na siasa zake kwani yeye ana watu wenye ushawishi mkubwa na pia wenye pesa nyingi, hivyo watashinda. Na hapo akamwambia kuwa mzee Matata atakuwa nyuma yake kuanzia hatua ya kwanza hadi ya mwisho watakapokuwa wakipongezana wakiwa ikulu huku yeye akiwa ni raisi. Kumsikia mzee Matata pekee haikutosha kumshawishi Mathias kukubaliana na wazo la raisi. Kitu kikubwa kilichokuwa kinamkwamisha katika hilo ni ukaribu aliokuwanao kwa John Masele kuanzia chuo kikuu walipokutana, John akawa raisi wa chuo huku Mathias akiwa makamu wake. Ukaribu huu ukaunda kama undugu, na hatimaye wakajiunga na chama tawala. Sasa John ni waziri wa mambo ya ndani na nje wakati yeye ni waziri wa nishati na madini. Raisi anataka kuwafanya maadui kwa mara ya kwanza!!! Mathias hatimaye anashawishika, waandishi wa habari wanaitwa katika mkutano. Mathias Obhare anatangaza nia ya kuwania nafasi ambayo John Masele alikuwa anawania. Kujitangaza kwa Mathias Obhare kulimshtua sana Masele, akajiuliza ni lini Obhare akawaza upinzani kama ule. Kwanza ni yeye alikuwa wa kwanza kumshawishi atangaze nia, in akuwaje sasa na yeye atangaze nia. Si bure kuna kitu hapa! akajisemea Na hapo akatambua wazi kuwa kuna hila imefanyika dhidi yake ili asiweze kuleta mapinduzi kwani alikuwa na misimamo tofauti kabisa na chama tawala japo naye alikuwa ndani yake. Kwa utulivu kabisa akaamua kukutana na Obhare na kumshawishi asigombee nafasi ile kwa sababu kwa namna moja ama nyingine ingeweza kuwaingiza katika malumbano makubwa na kuutia doa urafiki wao. Akamsihi kuwa iwapo ataachia nafasi ile basi atamchagua kuwa makamu wa raisi kama walivyofanya wakati wakiwa chuo kikuu Obhare hakutoa jibu palepale, akayafikisha yale yote kwa raisi. Mtukufu Raisi akatumia huo mwanya kuanza kumchafua Masele mbele ya wananchi. Akasambaza maneno makali kwa wajumbe juu ya uoga wa kushindwa alionao Masele pia akaelezea juu ya tamaa ya madaraka aliyokuwa nayo bwana yule. Na hapo baraza la chama tawala likatangaza rasmi kuliondoa jina la waziri wa mambo ya ndani na nje katika kinyang’anyiro kile. Fukuto likaanzia hapo! Baada ya juma moja, jambo jingine kubwa likazuka. Mathias Obhare akatekwa na kuibiwa gari lake kisha akapigwa sana. Kipigo kilichosababisha akimbizwe Afrika kusini upesi kwa ajili ya matibabu. Zikasemekana ni hila za Masele baada ya kuzidiwa kete na mpinzani wake kisiasa. Baraza likaketi tena na kumweka kitimoto Masele ambaye alikataa kata kata kujihusisha na tukio lile, huku akisisitiza kuwa amebariki bwana Obhare kuwania kiti kile. Lakini maneno yake hayakutosha kutengua kilichokuwa kimepangwa tayari. Akiwa ameketi nyumbani na familia yake, mara akaisikia taarifa ya habari kuwa Raisi amemvua nyadhifa za uwaziri wa mambo ya ndani na nje….. huku sababu kuu ya kufanya vile ikisemekana ni kwa maslahi ya wananchi na sio chama. Jina la Masele likazidi kuchafuka huku Mathias Obhare akianza kukaa katika damu za raia wema. Wachache wenye kujitambua walihisi kuna jambo linatokea hapo katikakati. Lakini hawakuwa na pa kusemea. Lakini mtanzania mmoja ambaye alikuwa masomoni nchini uingereza alitamani sana amalize masomo yake ili aweze kuingia katika upelelezi juu ya kipi kinachotokea maana naye alitilia mashaka matukio yale mfululizo. Huyu alikuwa ni Steven Marashi, mwanausalama wa taifa aliyekuwa ameenda kuongeza elimu yake nchini uingereza. Akiwa huko akajiunga katika vikundi vya kiafrika vya kucheza ngoma na kufanya michezo ya majukwaani, fani aliyokuwa akiipenda tangu utoto wake alipokuwa shuleni. Fani ikanoga na kung’ara zaidi katika ukubwa wake. Aliporejea nchini Tanzania, akaingia rasmi katika sanaa ya maigizo. Ungeanza vipi kujua yule bwana alikuwa mwanausalama wa taifa na mpelelezi aliyekubuhu? Safari ikaanzia hapo!!! Alipojiunga na sanaa mtu mmoja tu ndiye aliyejua ni kwanini anajiunga katika sanaa, huyu alikuwa ni rafiki yake kikazi na hatimaye hadi mtaani wakawa marafiki na kushirikishana mambo yao mengine. Alikuwa ni Yakubu Gama, zao la usalama wa taifa lenye asili ya Naijeria lakini mwenye uraia halisi kabisa wa Tanzania kwa kuzaliwa. Na baada ya miaka minne Steven anakufa katika mazingira ya kutatanisha!!! Na baada ya kifo chake mambo mengi yanajitokeza hapo katikati, Gama hakupata hata fursa ya kuonana na Sam yule mwandishi ambaye alikuwa rafiki wa karibu sana wa Steve! Hadi usiku ule aliokwenda kumwekea dhamana. Dhamana iliyotoka wa mtukufu raisi moja kwa moja, kupitia amri ya IGP. Dhamana iliyokuwa na makusudi ndani yake! Kuna kitu kilikuwa kinatafutwa na Sam alidhaniwa kuwa anaweza kuwanacho ama kuwezesha kupatikana kwacho! Ni kitu gani hicho? Hili swali linabaki katika kichwa cha Yakubu Gama ambaye yu hai sasa lakini akiwa amejeruhiwa! Yakubu Gama anaapa kuwa atapeleleza hatua kwa hatua hadi ajue ni kitu gani kilimuua Steve! Huenda katika utafiti huo akatambua pia ni nani anayeitwa BVB. ****
HILA NO.10
SEHEMU YA KUMI Taarifa za vifo vya mapacha wawili tegemeo kabisa katika ngome ya mzee Matata ilipokelewa katika namna ngeni kabisa na mzee yule, alikuwa amepagawa na hakutarajia hata kidogo jambo kama lile lingeweza kutokea. Hakuamini hata kidogo kama Sam angeweza kukabilia na vijana wale machachari na kisha yeye akaibuka bingwa. Tena sio bingwa wa kawaida tu, bingwa aliyeua. Upesi akachukua simu yake na kumpigia mzee Robert, mrakibu mkuu wa polisi. Simu ilipokelewa kwa utulivu! Harakaraka na kwa papara kubwa Matata alianza kumuhoji Robert juu ya tukio lililojitokeza Sinza hotelini. “Kwani kuna tatizo gani mzee Matata ya nini kuuliza kila kitu kinachohusu usalama wa raia na hasahasa siri za jeshi la polisi. Samahani lakini kwa namna moja ama nyingine nashindwa kukuelewa mkuu….” Bila kujibu chochote mzee Matata akakata simu. Robert akabaki kutetemeka asijue mzee yule alichukulia vipi maelezo yale aliyompa. Lakini alifanya vile kwa sababu alilazimika kufanya, kwanza alikuwa amevurugwa sana. Matukio yalikuwa yanapangana, kabla hili halijaisha anasikia jingine likipanda juu yake. Ilikuwa lazima achanganyikiwe na matukio yale yaliyozungukwa na utata. Akiwa anaanza kusahau juu ya simu aliyozungumza na mzee Matata, mara simu yake ya mkononi ikaita. Alikuwa ni IGP….. Robert akaomba dua zote kabla ya kuipokea simu ile kwa sababu alimjua vilivyo mkuu wake wa kazi. “Robby, hivi ungemjibu mzee Matata vizuri ni kitu gani kingekupungukia labda…… Robby, mzee Matata akiongea na mkuu wan chi ujue utaingia matatani. Nisikilize Robby, wewe na mimi tunafahamu ni pesa kiasi gani mzee Matata ametoa ili kufadhili kampeni za chama. Unajua ni jinsi gani mzee Matata na raisi ni marafiki, chunga sana mdomo wako Robby, chunga sana inaweza kukugharimu, nimekusihi haya kwa sababu wewe ni mzazi na una familia kubwa… sitaki familia yako iteseke. Nadhani unanielewa, sasa mpigie simu mzee Matata tena ni muda huu na umwombe msamaha….” Alihitimisha IGP. “What? Ni nini hiki IGP… Msamaha kwa kuficha siri za jeshi letu mkuu…” “Nimesema mwombe msamaha. Nimemaliza…” akakata simu IGP. Robert Massawe akabaki kuitazama simu ile kana kwamba ina lolote la kumshauri ama inaweza kushiriki naye katika mshangao mkubwa aliokuwanao… lakini haikuwa hivyo. Simu nayo iliendelea kumtazama. “Si bure…..” Robert alijisemea huku akiichukua simu yake na kubofya jina la mzee Matata. Funika kombe mwanaharamu apite!! Alijisemea huku akiungoja upande wa pili uweze kupokea simu. Simu iliendelea kuita bila kupokelewa!! ***** WAKATI simu ya mzee Matata ikiita, mzee huyu alikuwa ameenda mahali kujipooza hasira zake. Kitendo cha kukatiwa simu ya Robert alichukulia kama dharau kubwa sana kwake na tena ikiwa imefanywa na mtoto mdogo asiyekuwa na uwezo wa kutoa kauli yoyote mbele yake. Mzee Matata alikifikia chumba alichokusudia akakifungua na kukabilia na sura iliyokuwa ikisihi huruma. Sura ya kike iliyopauka haswa na kuchubuka kutokana na kipigo. Macho yake makubwa yalikuwa yamedumbukia ndani na midomo yake ilikuwa mikavu. “Bitch! Huyo hawara wako anashirikia na watu gani?” Matata alitupa swali. Yule binti aliyezidi kusihi huruma kwa yale macho yake tu alijitahidi aseme lolote lakini akashindwa. Akabaki kulishika koo lake na hapo sauti ya kukoroma ikamtoka. “Nina kiuuu…” Hakika alikuwa ana kiu, kiu kikalikausha koo na kuondoka na ile sauti yake nzuri. Sauti iliyompagawisha Sam na kujikuta akiamua kutangaza ndoa kabisa. Alikuwa ni Christina Elisha Prosper ama alivyozoeleka kwa wengi kama Tina! Ile hali ya Tina kulalamika kiu badala ya kujibu swali aliloulizwa ilimghafirisha tena mzee Matata, akahisi anazidi kudharauliwa na watu wasiostahili hata kupita njia anayokanyaga yeye. Mzee Matata akaondoka, sura yake ikiwa nyekundu akaingia bafuni na kutoka na ndoo iliyojaa maji. Akaifikisha katika chumba alichokuwa amehifadhiwa Tina. “Inama unywe maji kisha unijibu…” mzee Matata akamweleza Tina kwa sauti iliyojaa upole. Tina akajisogeza kwenye ndoo na kuinama kama mbuzi. Akaanza kunywa maji. Mzee Matata akamvamia pale pale kwenye ndoo na kukishika kisogo chake na kumzamisha kichwa kizima katika ile ndoo. Tina alitapatapa akirusha miguu huku na kule, alivuta maji kwa pua na midomo. Akazikosa pumzi zake. Baada ya dakika mbili mzee Matata akamwachia. Tina akabaki kutapika huku na kule, akizisaka pumzi kwa jitihada kubwa, katika kuruka huku na kule mara akamtapikia mzee Matata katika mguu wake. Yule mzee asiyekuwa na huruma akamnasa kibao kisha akamfyatua teke kali tumboni huku akimsindikiza na matusi. Tina akatua katika kingo ya ukuta, uso ukabaki kutambaa sakafuni na maneno yasiyoelewekaeleweka yakimtoka. “Sam anashirikiana na nani katika kikundi chake cha kijasusi??” alihoji mzee Matata. “Sijui lolote…. Najua ni mwandishi tu…..” alilalamika Tina. Mzee Matata akataka kumrushia adhabu nyingine ya teke lakini safari hii akaisikia simu yake ikiita. Akaufunga mlango na kutoweka. Akaipokea simu na kuupokea msamaha kutoka kwa Robert. Mrakibu msaidizi wa jeshi la polisi!! Ile hali ya kuombwa msamaha ikampunguzia ghadhabu kidogo na kujiona mtukufu sana mbele ya watu wenye madaraka. “Haya kijana…. Ni nani wale waliopambana na kuuana katika hoteli ya Sinza…” akamuhoji Robert kifedhuli. “Wawili hawajajulikana majina lakini mmoja ni kijana wetu…” alijibu Robert huku akiuma meno yake kwa hasira. “Na kijana wenu naye amekufa?” aliuliza. “Haijathibitishwa bado lakini yupo mahututi hospitali ya jeshi Lugalo…” “Ok! Vizuri ntakupigia baadaye nikihitaji kujua juu ya hali yake. Poleni na muwe na siku njema…” akaaga na kukata simu. “Fuck!” alifoka Robert huku akiibamiza meza iliyokuwa pale ofisini, akaituliza akili yake na kujiuliza juu ya yule mzee ambaye anatambulika nchini kwa biashara zake kubwa anazomiliki. Sasa kulikoni mambo hayo ya jeshi awe anayafuatilia kwa ukaribu kiasi hicho. Lazima kuna kitu hapa!! Alijishauri, na kisha akajiapiza kutothubutu kufuatilia nyendo za mzee Matata. Hakutaka kuyapata matata!! Akakumbuka maneno kadhaa ya IGP alipokumbushwa juu ya familia yake, hapo uoga ukamwingia. Lakini hakuwa amejitoa katika vita na mzee Matata kama alivyodhania!! Nd’o kwanza alikuwa anaikaribia. *** SIMU yake iliyokuwa katika mfumo wa mtetemo iliunguruma mara tatu kabla mkewe hajamgutusha kutoka usingizini. Robert Masawe alijinyoosha kidogo kabla ya kutazama kwenye kioo na kukutana na namba mpya. Hilo halikumshtua ilikuwa kawaida kupewa taarifa kadha wa kadha kutoka kwa wakuu wake ama wadogo zake kikazi kwa kutumia namba mpya. “Jambo afande, CW00JT Lugalo hospitali..” alijitambulisha kwa namba yake na Robert akatambua kuwa kuna ujumbe anatakiwa kupokea. “Endelea afande.” “Kuna vijana watatu wanahitaji kumwona Inspekta Yakubu Gama….” “Vijana? Vijana kutoka wapi?” “Madaktari wameagizwa na mzee Matata!” “Whaat? Madaktari, madaktari kivipi?” “Sina nijualo zaidi ya kukupa hii taarifa afande..” “Usiwaruhusu kwanza!” akaagiza na kukata simu. Akatulia kitandani kwa sekunde kadhaa, mkewe naye akaketi kitako kuungana na mumewe. Hakutaka kumuuliza lolote, zaidi alibaki kumminyaminya begani kama namna ya kumfariji. Robert Masawe, mrakibu msaidizi wa polisi aliitwaa tena simu yake wakati anataka kupiga mara ikaingia simu kutoka kwa mzee Matata. Robert akaruka sentimita chache kutoka katika kitanda, ni kama alikuwa ameona mdudu wa hatari. Hakuipokea simu ile akaiacha iite hadi pale ilipokatika. Na hapo Robert akampigia IGP. “Jambo afande!” akasalimia. IGP hakujibu akaendelea kumsikiliza. “Mkuu, Mzee Matata ameagiza madaktari kwa ajili ya Inspekta Yakubu Gama! Unayo taarifa hiyo?” “Unawezaje kupata taarifa nzito kama hiyo kabla mimi sijaipata?” IGP akajibu katika mfumo wa swali kwa swali. Jibu ambalo lilimkera Robert lakini hakuwa na la kufanya. “Lakini mkuu ulipaswa kunieleza kwa sababu vijana walio katika lindo wanatoa taarifa kwangu kama ulivyoagiza mkuu…” “Kwa hiyo unamaanisha waanze kuripoti kwangu moja kwa moja?” “Hapana afande!!” “Waruhusu waingie nimezungumza naye, ametusaidia madaktari kutoka India wanusuru uhai wa Gama…. Wakati mwingine tabia yako ya kupenda kuuliza kila kitu siku ya siku utasababisha tukose misaada….” Akamaliza na kukata simu. Super retendant Robert Masawe akapagawa! Na hapo mkewe akaamua kuhoji kulikoni, Robert Masawe alijaribu kumkwepa mkewe lakini mwanamke yule hakukubali kabisa. Akakazia hadi Robert akasalimu amri akaketi kitako na kuanzia kumsimulia mkewe juu ya mkasa mzima unaoendelea. Mkewe alikuwa makini sana kumsikiliza na baada ya maelezo yale, mkewe akatokwa na kauli ambayo bwana Robert hakuitegemea. “Ukilala usingizi basi Gama atalala usingizi wa milele leo, pindi utakapoamka utakutana na lile neno kwamba jitihada za madaktari zilishindikana…. Hakuna madaktari hapo mume wangu, hao ni watu wabaya na hapo wanataka kumzimisha Gama ili asiseme ambacho amekigundua huko alipotoka…” “Heh! Mke wangu umeyajuaje haya yote?” “Nasoma sana riwaya mume wangu hasahasa za kipelelezi, wewe hupendi riwaya lakini zile za wakongwe zina mambo mengi ya kujifunza, mfano Mhanga wa ikulu ya Beka Mfaume, Mkimbizi ya Hussein Tuwa na Msako wa Hayawani ya Eddie Ganzel…. Naona wanayoyaandika nd’o kisa kama hiki, ukitaka kuamini we lala halafu asubuhi tutasimuliana…. Lakini uhai hautakuwepo tena. Gama atakuwa mfu!!” Maneno ya mkewe yakamsisimua Robert licha ya kutokuwa na undugu wowote na Gama lakini alitambua kuwa nchi ilikuwa ikimuhitaji sana kijana shupavu kama yeye ili amani iendelee kuwepo huku waovu wakifikishwa mbele ya sheria. Uzalendo ukajikita katika moyo wake, ujasiri ukajiunga naye upya. Akaona si sawa kumpoteza Gama katika namna nyepesi hivyo. Alitambua kuwa vijana waliokuwa wameweka ulinzi kwa Gama wasingeweza kuwaruhusu wale madaktari kuingia katika chumba cha mgonjwa bila idhini yake yeye. Pale pale akachukua simu ya mkewe akabofya namba za mmojawapo wa askari katika lindo la hospitali ya Lugalo ambayo alikuwa amehifadhiwa Gama. Akamwambia asogee kando kabisa waweze kuzungumza. “Naomba uende katika chumba alicholazwa Gama, kamtazame hali yake na ukiwa humo chumbani nipigie simu.” Akamaliza na kukata!! Yule kijana kama alivyoamrishwa akawapita wale madaktari ambao walikuwa wakingoja ruhusa, akaingia katika chumba alichokuwa amelazwa Gama. “Hali yake bado si salama amepoteza fahamu bado..” “Afande! Sina imani hata kidogo na hao madaktari, ni mimi nakueleza wewe tu na ujue wewe tu kwa sababu kanuni za jeshi kumtilia mtu mashaka ni nguzo kuu katika upelelezi. Hivyo nakuomba ufanye kitu kimoja…… ni cha hatari lakini nd’o inaweza kuwa salama yetu…. Wasiliana na daktari mmoja anaitwa Haji. Ni rafiki yangu sana kisha nipe nizungumze naye. Mengineyo nitakujuza. “Sawa afande!” alijibu yule kijana kisha akatoweka. Akafanya kama alivyoamriwa! ****
HILA NO.9
SEHEMU YA 9 WAKATI Sam anapiga simu ile hewa kuna makundi mawili sehemu mbili tofauti yalikuwa yametulia tuli kusikiliza anachokizungumza Sam, kila kundi lilipagawa katika namna ya kipekee. Kundi moja lilikuwa katika ofisi isiyokuwa rasmi iliyokuwa imejazwa na wanausalama wa taifa wanne. Simu ile iliwapa tumaini na kisha kuwapa swali tena juu ya huyo Tina. Tina ni nani na amechukuliwa na nani, mwanausalama mmoja akamtambua Tina kama mchumba wa Sam. Na pia akazitambua taarifa za kupotea kwake ambazo zilikuwa vituo kadhaa vya polisi. Hilo wakalipuuzia na kutilia maanani juu ya mzigo ambao Sam alikuwa akitarajia kumpa mtu wa kuitwa Masu, kwa jinsi walivyolinasa jina lake katika vinasa sauti. Mkuu wa usalama wa taifa akampendekeza kijana wake mahiri kabisa katika kufuatilia kimyakimya, asiyeogopa kufa na asiyetambua nini maana ya kusamehe! Yakubu Gama akapewa jukumu hili . Na ni huyu ambaye aliagizwa kutega vinasa sauti katika nyumba ya Sam awali. Gama alifikishiwa taarifa hii akiwa anajiandaa kuandika barua ya kuomba likizo, hivyo wazo la likizo likaishia palepale. KUNDI la pili lilikuwa kundi la Mzee Matata, hawa waliipokea taarifa ile kwa shangwe hasahasa baada ya kusikia juu ya mzigo ambao Sam alikuwa akiumiliki. Ni hili walikuwa wakilitafuta siku zote, na hata uamuzi wa kurudisha vinasa sauti katika nyumba ya Sam ulikuja baada ya kukosekana mtu mwingine wa kumhisi juu ya umiliki wa mzigo ambao walikuwa na mashaka nao tangu awali. Mzee Matata akafanya tabasamu la ushindi baada ya kupokea taarifa zile, safari hii alikuwa na vijana wapya baada ya wale waliotorokwa na mama lao kuambulia kupigwa risasi na kupoteza maisha. Akawapendekeza vijana wake wawili aliokuwa akiwaamini sana katika suala zima la kupeleleza. John na Johnson ama walivyozoea kuitana ‘PACHA’. Na hakika walikuwa pacha, wote walikuwa na roho mbaya, wote walikuwa wartefu waliojaa miili yao kimazoezi na kubwa zaidi wote walikuwa hawachoki kuua, inapobidi na wakati mwingine hata isipobidi. Kwao kuua ilikuwa mojawapo ya burudani!! Na ni hawa waliofyatua risasi kuwasambaratisha wale wanyakyusa wawili baada ya kutorokwa na mwanamke wa shoka MAMA LAO. **** HAIKUWA saa mbili usiku kama Sam alivyoongea katika simu hewa. Badala yake ilikuwa saa tano asubuhi, akalipia chumba namba kumi na nane, akaingia katika kile chumba kisha akatoka baada ya kufanya alilopanga kufanya kwa umakini. Alirejea majira ya saa kumi jioni akiwa amevaa miwani na kofia ya pama huku miguuni akiwa amevaa viatu maarufu kwa jina yeboyebo. Ilikuwa ngumu sana kutambua kuwa yule alikuwa ni Samwel Mbaule. Akajiweka mahali ambapo angeweza kumwona kila mtu aliyekuwa akiingia na kutoka ndani ya hoteli ile ambayo ilikuwa imejitenga mita kadhaa kutoka barabarani. Nia yake ikiwa kumtambua adui yake ni nani aweze kuanza vita ya kimyakimya. Vita ya kumwokoa Tina iwapo yu hai, na pia kumweka huru mama lao dhidi ya hila aliyofanyiwa na kisha kutangazwa kuwa ni muuaji. Akiwa anakunywa soda yake taratibu, jicho lake liliendelea kuwa makini kabisa kutazama yeyote ambaye ataingia pale na kutoka walau atazame iwapo kuna sura anaweza kuifananisha. Muda ulizidi kusogea lakini hakuambulia sura yoyote. Akaanza kukata tama huku akihisi mama lao hakuwa na uhakika wowote juu ya watu kuingia katika awamu mbili na kuweka vinasa sauti katika nyumba yake. “Huenda mama lao alikuwa ameghafirika tu!!” Sam alijisemea huku akiimalizia soda yake ili aweze kuondoka na kuingia katika chumba kile alichokilipia. Sam alisimama kinyonge kabisa huku kichwa kikimuuma, alijiona kuwa hana mbinu mbadala za kumjua adui yake kama ambavyo mama lao alimpamba kuwa anaweza kuwa. Taratibu kabisa akafika mapokezi na kuchukua funguo za chumba chake. Akajiondokea huku akili ikimchemka vibaya mno. Alipoifikia lifti alibaki akijiuliza ni kipi sahihi, kupanda ngazi ili apoteze muda ama apande lifti awahi chumbani bila kuwa na sababu yoyote ya kuwahi? Wakati anajiuliza mara lifti ikafunguka na mtu mmoja akatoka, Sam akafikia maamuzi ya kuingia ndani ya lifti. Akaiamuru imfikishe ghorofa iliyokuwa na chumba chake. Ndani ya sekunde kadhaa mlango ukafunguka kumaanisha kuwa alikuwa amefika eneo stahiki. Taratibu Sam akaanza kuambaa katika korido ili aweze kukifikia chumba chake. Na mara akapatwa mshtuko mkubwa sana baada ya kusikia mlipuko mkubwa, si yeye tu bali wateja takribani wote waliokuwa vyumbani walikurupuka, wengine wakiwa uchi na wengine wakiwa na mavazi ya kulalia. Wanawake kama kawaida yao walikuwa wanalia kwa sauti za bila kujua ni kitu gani kimejiri….. **** Alikuwa ni Yakubu Gama ambaye alikuwa wa kwanza kuingia katika chumba ambacho Sam alikuwa amekilipia kwa ajili ya kukutana na mtu hewa waliyezungumza naye kwenye simu. aliingia katika chumba kile hata kabla Sam hajaingia na kutoka baada ya kukilipia. Hivyo wakati Sam anaingia hakuwa peke yake, Gama alikuwa yu ndani tayari. Waliofuata kuingia katika kile chumba walikuwa ni PACHA kutoka kwa mzee Matata. Alitangulia John kisha Johnson, wakati huo Gama akiwa uvunguni. Nia yake ikiwa ni kutoka katika ficho lile punde baada ya wawili hao walioingia kukabidhiana huo mzigo, aliiweka sawa bastola yake vyema katika kiwambo cha kuzuia sauti. Kisha akaendelea kutulia. Wawili wale ambao aliamini kuwa ni Sam na mwenzake (Masu) hawakuzungumza lolote badala yake walianza kupekua huku na kule kisha mmoja akaingia bafuni na hakutoka huko. Gama akiwa uvunguni akabaki katika mshangao lakini hakupoteza umakini wake, akayakaza macho yake vyema bila kuruhusu mtikisiko wa aina yoyote. Mara yule bwana mmoja aliyebakia akaingiza mikono yake uvunguni na kuanza kupapasa. Gama akawahi kuuondoa mguu wake ambao ungeweza kuguswa na yule bwana….. Baada ya kupapasa mara yule bwana akainama uvunguni. Ebwana! Macho kwa macho na Gama. Gama hakumwachia upenyo maana alijua tayari mambo yameharibika. Gama akafyatua teke, lakini kama ilivyo maaajabu… yule bwana akauondoa uso wake ndani ya nukta chache, Gama akajikuta amebutua teke kitanda. Na palepale akawahi kujitoa uvunguni, lakini kabla hajasimama imara akajikuta akipokea teke kali sana usoni, akayumba lakini hakuanguka akajiweka imara akasimama wima. Ana kwa ana na kipande cha mtu!!! Gama hakuonekana kuwa na mwili wa kimazoezi, alikuwa mnene kiasi na anayeonyesha kuwa legelege, jambo hili lilimzubaisha Johnson. Akamchukulia Gama kuwa ni dhaifu, akamsogelea ili amkwide, lakini akakutana na pigo kali la karate katika shingo yake na kisha ngumi kali katika korodani zake. Yule bwana mkakamavu akajikuta amelainika, hakika alikuwa amekutana na mtu kati ya watu! “Pachaaa…” akapiga kelele za hofu baada ya kuona amezidiwa, na hizi zilikuwa kelele zake za mwisho kabla Gama hajafyatua ngumi kali iliyojikita katika shingo yake na kumtupa chini ambapo hakuwahi kuamka tena milele. Wakati akipambana kuvuta pumzi za mwisho mara chumba kikavamiwa na Johnson, yule pacha ambaye alikuwa bafuni, hakuuliza swali akamvamia Gama kwa papara akamnyuka ngumi mbili tatu za harakaharaka. Gama akajituliza kwa umakini zaidi akamuhesabia hatua Johnson alipojisogeza tena Gama naye akafyatuka na kuanguka naye chini mzimamzima. Akamkaba shingo kwa uimara kisha akamuuliza juu ya wapi ulipo mkanda. Johnson hakujibu chochote kwa sababu alikuwa amepigwa kabali, Gama akalitambua hilo, upesi akamwachia na katika nukta iliyofuata akampiga ngumi nzito kwenye taya. Johnson akajiharishia!! Na hapo akakiri kuwa alikuwa anapambana na kiumbe wa ajabu kupita wote aliowahi kukutana nao katika maisha yake. “Ni nani alimuua Steven?, Tina ni nani?, na mkanda upo wapi… “ “Sijui lolote mkuu, nimeagizwa tu…” alijibu huku akigumia kwa maumivu makali. “Jina la aliyekuagiza.. upesi kabla sijainyonga shingo yako bwana mdogo…..” akatoa karipio kali Gama. Macho yake yakiwa mekundu na mikono ikiwa na tamaa kali ya kuua!! “BVB” “BVB ni nini maana yake.. upesi….” Alihoji huku akiikaza shingo ya yule bwana. Hilo likawa swali la mwisho kabisa kuuliza kabla yule bwana hajafanya kitendo cha ajabu, akaanza kujinyonga nyonga kama anayeugulia tumbo. Na mara mlipuko mkubwa ukasikika. Hapo ndipo kilipozuka kizaazaa!! Gama akarushwa mbali kabisa na mlipuko ule. Mlipuko ambao hakuutegemea katika mazingira yale! Mlipuko ule ukawavuta watu waliokuwa nje na ndani ya hoteli ile akiwamo Sam. Na hakuwa Sam pekee bali askari kanzu wapatao kumi waliomsindikiza Yakubu Gama wakaingia kazini. Kwa papara kama kawaida yao!! Utawajua tu kwa amri zao. Wakatapakaa huku na kule, raia nao wakakimbilia eneo la tukio, Sam akaongoza mbio hizo akawa mmoja kati ya watu waliowahi kuwasili eneo la tukio. Macho yake yakakutana na mwili wa Yakubu Gama katika chumba chake. Sura na umbo havikuwa vigeni kabisa katika macho yake. Sam alijiuliza ni wapi aliwahi kumwona kiumbe yule, akaituliza akili na kujikuta akimkumbuka. Alikuwa ni yule mwanaume aliyekuja kumwekea dhamana na kisha kumsihi awe makini. Dhamana ya maajabu ya usiku mnene sana. Inakuwaje bwana huyo katika chumba chake? Ilistaajabisha. Na hapo akajipongeza kwa kujisajili kwa jina lisilokuwa lake wakati anaingia hotelini hapo. Kwani kwa tukio lile tayari ni kizaazaa kipya. Sam akazidi kutambua kuwa lipo jambo ambalo limetanda katika mkasa wa kifo cha Steven Marashi na hata baba yake mzazi. Kichwani akajiwekea picha kuwa kuna pande zaidi ya moja zinawania mkanda ambao alikuwa anaumiliki! Pande hizo ni zipi? Alijiuliza bila kupata jawabu!! Katika purukushani za hapa na pale kabla polisi hawajaweka utando wao wa kuzuia raia kuingia ndani ya kile chumba, Sam alifanikiwa kukitoa kinasa sauti chake ambacho alikiweka baada ya kuingia katika chumba kile na kutoka majira ya saa tano. Kilikuwa kimewekwa katika godoro ambalo alikuwa amelichana na kisha kukitandika kitanda vyema. Sam alizuga kuwa amesukumwa, akaangukia pale na kwa sekunde chache akaondoka na kile kifaa. Wakati anaondoka alipishana na yule mwanadada aliyemwandikisha kuingia katika chumba kile. Yule dada bado hakuwa na uhakika kama yu sahihi ama la. Sam mwenye hofu akajikaza akaongeza mwendo. “We kaka…” yule dada akajaribu kuita. Sam hakugeuka. “Ni yeye jamani…” sauti ikasikika kama akiwaambia watu fulani. Sam akawa ameifikia kona, akaanza kukimbia, akakata mitaa hapa na pale hadi akatokea Ubungo. Jasho lilikuwa linamtoka haswa. ***